Powered By Blogger

Translate

Sunday, June 30, 2013

OBAMA AFRIKA KUSINI

tukio ya Afrika

Obama : Igeni mfano wa Mandela

Rais Barack Obama wa Marekani Jumamosi(29.07.2013) amewashajiisha viongozi wa Afrika na duniani kwa jumla kufuata mfano wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela kwa kulitanguliza mbele taifa kabla ya nafsi yake.
Obama amesema wakiwa kama viongozi wanashikilia nyadhifa hizo kwa muda na wasidanganyike kiasi cha kufikiri kwamba hatima ya nchi yao haitegemei kadiri watakavyoendelea kuwa madarakani.
Obama alikuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliomjumuisha pia Rais Jacob Zuma mjini Pretoria akiwa katika ziara yake ya wiki moja barani Afrika ambayo tayari imemfikisha Senegal na anatazamiwa kuzuru Tanzania hapo Jumatatu. Obama anafanya ziara hiyo wakati nchi nyingi za Kiafrika zikiwa kwenye mizozo ya kidini, kikabila na mengineyo.
Sio wakati muafaka kuzuru Kenya
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Obama ameamuwa kukwepa kuizuru Kenya kwa sababu ya nchi hiyo kuhusika kwenye mzozo wa kimataifa. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imemfungulia mashtaka Rais Uhuru Kenyatta kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu yakiwemo mauaji kuhamisha watu kwa nguvu, ubakaji,ukandamizaji na vitendo vya kinyama vilivyofanywa na wafuasi wake kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Obama amekaririwa akisema "Wakati sio muafaka akiwa kama rais wa Marekani kuitembelea Kenya wakati masuala hayo yakiwa bado yanafanyiwa kazi na nataraji yatapatiwa ufumbuzi." Amesema tayari ametembelea Kenya mara kadhaa na ataitembelea tena nchi hiyo kipindi cha usoni.
Obama na Zuma walikuwako kwenye Majengo ya Umoja ambako ndiko kuliko ofisi za serikali na ndiko mahala ambapo Mandela alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini hapo mwaka 1994 baada ya kuwa gerezani kwa miaka 27 kwa harakati zake za kupambana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo.
Rais Barack Obama wa Marekani na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini katika mkutano na waandishi wa habari (29.06.2013). Rais Barack Obama wa Marekani na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini katika mkutano na waandishi wa habari (29.06.2013).
Mandela mwenye umri wa miaka 94 amelazwa katika hospitali mjini Pretoria kwa wiki tatu sasa kutokana na maambukizi ya mapafu. Zuma amewaambia waandishi wa habari hali ya Mandela ni mbaya lakini imara na kwamba taifa zima linamuombea apone.
Obama na mke wake wamekutana na baadhi ya ndugu wa familia ya Mandela lakini kutokana na matakwa yao hakupanga kumuona Mandela ambaye ni mmojawapo wa watu adhimu kabisa duniani.
Obama akimtaja Mandela kwa jina lake la kiukoo amepongeza mjumuiko wa kijamii wa Afrika Kusini kutoka utawala wa kibaguzi na kusema kuwa ni alama inayon'gara duniani.
Mandela shajiisho la dunia
Nelson Mandela alama ya mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi. Nelson Mandela alama ya mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi.
Obama amesema mapambano dhidi ya utawala wa kibaguzi kwa ajili ya uhuru,moyo ya uadilifu wa Madiba kipindi cha nchi cha kihistoria cha taifa hilo kubadilika na kuwa huru na la demokrasia yamekuwa ni mambo yaliomshajiisha yeye mwenyewe binafsi na kuwa kichocheo kwa dunia.
Zuma amemwambia Obama kwamba yeye na Mandela wamefungamanishwa na historia kwa kuwa marais wa kwanza weusi kwa nchi zao na kwa kuwasilisha matumani ya mamilioni ya watu barani na Afrika na wale wanaoishi nje ambao huko nyuma walikuwa wakikandamizwa.
Katika masuala mengine Obama amekataa kujifunga moja kwa moja katika kuunga mkono juhudi za Afrika Kusini kuwania kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Amesema mfumo wa Umoja wa Mataifa unahitaji kurekebishwa na litakuwa sio jambo la kawaida kulitanuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bila kujumuisha uwakilishi wa Afrika.
Uwekezaji wa China haumtishi
Rais Barak Obama katika mkutano na waandishi wa habari Pretoria (29.06.2013). Rais Barak Obama katika mkutano na waandishi wa habari Pretoria (29.06.2013).
Obama pia amesema anataka kuimarisha biashara na Afrika na kuanzisha mazungumzo mapya ya mkataba wa biashara na Afrika ili kuuboresha kwa kampuni za biashara za Marekani.Pia amesema anakaribisha juhudi kubwa zinazofanywa na nchi nyengine kutafuta fursa za biashara barani Afrika ikiwemo China.
Amesema hatishwi na jambo hilo na anafikiri ni zuri ila tu ushauri wake ni kuhakikisha tu kwamba ni kwa ajili ya manufaa ya Afrika kwa kuhakikisha miradi ya uwekezaji ya kigeni inawaajiri Waafrika,haindekezi rushwa au kuchukuwa rasimali zake za asili bila ya kuwafidia Waafrika.
Umuhimu wa Soweto
Kitongoji cha Soweto. Kitongoji cha Soweto.
Obama pia ametowa heshima zake kwa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini kwa kutembelea kitongoji cha Soweto ambapo amehutubia wanafunzi katika ukumbi wa jiji wa Chuo Kikuu cha Johannesburg.Takriban vijana 176 wameuwawa katika kitongoji cha Soweto wakati wa maandamano ya vijana dhidi ya marufuku ya utawala wa ubaguzi wa rangi ya kufundisha lugha za kienyeji za Kibantu.Uasi wa Soweto uliimarisha uungaji mkono wa kimataifa dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi na mwezi wa Juni hivi sasa unatambulika kuwa ni Mwezi wa Vijana nchini Afrika Kusini.
Obama atakamilisha ziara yake Afrika Kusini Jumapili ambapo anapanga kutowa hotuba kubwa kuhusu sera ya Marekani kwa Afrika katika Chuo Kikuu cha Cape Town na ataipeleka familia yake katika kisiwa cha Robben kuzuru gereza ambalo Mandela alitumikia miaka 18 ya kifungo chake cha miaka 27 gerezani.

MAPIGANO MAKALI KISMAYO

Wakaazi wa mji wa Kusini wa Somalia Kismayo wanaendela kukikmbia makwao, kutokana na mapigano makali kati ya mababe wa kivita katika eneo hilo.
Takriban raia kumi wameuawa katika mapigano hayo yaliyotokea siku ya Ijumaa.
Mji wa Kismayo ni mji muhimu wa kiuchumi Kusini mwa Somalia na vita hivyo vimechochewa na ushindani mkali wa kithibiti biashara katika mji huo wa bandari.
Ripoti zinasema wapiganaji wa kundi la Ras Kamboni wanaoongozwa na mbabe wa zamani wa kivita aliyejitangaza kuwa rais wa eneo hilo Ahmed Madobe walikabiliana vikali na wapiganaji wa waziri wa zamani wa ulinzi wa Somalia Bare Hirale, ambaye pia anaongoza kundi lingine la waasi katika eneo hilo.
Hali ya Utulivu imeanza kurejea tena mjini humo ambao ni ngome ya zamani ya kundi la kigaidi la Kiislamu la Al Shabaab ambalo lina uhusiano na kundi la Al-Qaeda.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo mara moja, na kutoa wito kwa mababe hao wa kivita kusitisha uhasama kati yao ili kuepusha maafa zaidi ya raia wasiokuwa na hatia.
Wanajeshi wa Kenyan wanaohudumu nchini humo chini ya muungano wa Afrika wanamuunga mkono Bwana Madodbe, lakini serikali ya Somalia halimtambui kama rais na pia haijakubali uamuzi wake wa kutangaza kuwa eneo hilo limejitenga na Somalia.

SUMAYE ATETA NA VIJANA

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amewatahadharisha vijana kuwa wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu wasikubali kupewa rushwa ya kanga, fulana na fedha na mtu yeyote anayetaka kuingia madarakani.
Akizungumza jana alipokuwa kwenye bonanza la michezo la kikundi cha Ukwamani Jogging kilichopo Kawe, alisema vijana wawe makini katika kuchagua mtu mwenye uwezo wa kuongoza ambaye atajali masilahi ya wananchi wake siyo kwa masilahi yake binafsi.
“Najiuliza kama ninajiamini nataka kugombea Kawe au Arusha au Sumbawanga kama ninafaa na wananchi wananiamini mimi ninafaa na wananchi wananihitaji kwa nini niwachochee kwa kanga au fedha ukiona hivyo huyo hawafai kuwaongoza,” alisema na kuongeza:
“Ukiona mtu anatoa kitu ili achaguliwe hafai kuwa kiongozi kwani uongozi ni mzigo,” alisema Sumaye.
Aliwashangaa watu wazima wanaochukua fedha na kuweka mfukoni kisha wanapita mitaani huku wakisema fulani anafaa kwa kuwa anatoa rushwa na fulani hafai kwa kuwa hatoi kitu chochote.
Sumaye alisema anayetoa fedha ili apewe kura huyo hafai kuwa kiongozi kwa sababu atakuwa anawatumikia watu wake waliompa fedha sio mwananchi ambaye alijitolea kumchagua kiongozi hiyo kwa kumpigia kula halali ili aweze kusaidia kumtatulia kero mbalimbali zinazomkabili.
Alisema kama kuna watu wanaumizwa kwa kuambiwa wanapokea au kutoa rushwa huku akiwa anaendelea na kufanya hivyo aache ili asiendelee kuumizwa na hilo.
Sumaye alisema nchi haiwezi kuwa na maendeleo kama viongozi wataendelea kudidimiza nchi kwa rushwa,ufisadi na kuingiza dawa za kulevya nchini.
Alisema viongozi wanaoleta dawa za kulevya kama ni nzuri wangezitumia lakini hawazitumii matokeo yake wanaoathirika ni vijana ambao wanategemewa kulijenga taifa hili.
“Hatuwezi kudidimiza jamii kwa kuwaletea dawa za kulevya ili watoto wa wenzao waharibikiwe kwa nini wasiwape au kutumia hao viongozi ili waathirike wao wenyewe?” alisema Sumaye.

WABUNGE WAINGANGANIA SSERIKALI

Dodoma. Wabunge wa CCM jana waliungana na Kambi Rasmi ya Upinzani kuing’ang’ania Serikali kwa kuupinga Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013/2014 uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa wakitaka kufanywa mabadiliko mbalimbali ikiwamo kuondoa ongezeko la kodi katika mafuta ya petroli kwa manufaa ya wananchi. Kadhalika, Kamati ya Bajeti imeonyesha kutofautiana na Waziri wa Fedha katika mapendekezo mbalimbali ya muswada huo ikitaka pia kupunguzwa kwa kodi ya mafuta, uagizaji magari huku mwenyekiti wa kamati hiyo akisema kuwa msingi wa mapendekezo yao ni kupunguza gharama za maisha na mfumuko wa bei kwa wananchi. Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda jana alipima upepo na kuamua kurudisha kwenye Kamati Muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria za Kodi, na sasa sheria hizo zitapitishwa leo bungeni badala ya jana. Muda mfupi baada ya kuanza kuchangiwa ndani ya Ukumbi wa bunge jana jioni, Makinda alisimama na kuwatangazia wabunge muswaada huo urudishwe tena katika kamati ambako wabunge waliokuwa wametoa mapendekezo ya marekebisho waliungana na Kamati ili kutoa ufafanuzi wa mapendekezo yao. Aidha wabunge hao pamoja na Spika wa Bunge waliusifu na kuunga mkono muswada mbadala uliowasilishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, uliosomwa na mbunge wa Viti Maalumu Christine Mughwai Lisu kwa niaba ya Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe. Mbali na kuitaka Serikali kuondoa ongezeko la kodi ya mafuta, simu, magari na kupunguza misamaha ya kodi walisema kuwa kitendo cha Serikali kutofuata ushauri wa wabunge kuhusu vyanzo vingine vya mapato, kinawazidishia maisha magumu Watanzania. Mapendekezo hayo ya wabunge, Kamati ya Bajeti na Kambi ya Upinzani yakipita yataweza kumpatia nafuu mwananchi wa kawaida, huku Serikali ikilazimika kujielekeza kwenye vyanzo vingine vya mapato vilivyoainishwa kwenye bajeti, wabunge wakivitaja baadhi kuwa ni pamoja na kodi katika kampuni za madini, kampuni za simu ili kutimiza malengo ya bajeti yake inayofikia Sh18.2 trilioni. Akichangia muswada huo ambao mjadala wake ulihitimishwa jana jioni, kabla ya leo Bunge kukaa kama kamati na kuupitia kifungu kwa kifungu Mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey zambi alisema: “Sikubaliani kabisa na ongezeko lolote la mafuta na dizeli, hayo yanaongeza moja kwa moja ugumu wa maisha kwa Watanzania.” Aliongeza akihoji: Serikali ya CCM ndiyo ipo madarakani, wananchi waliichagua kwa kura nyingi, sasa kwa nini izibe masikio kwa wananchi iliyowachagua? Iwasikilise basi, tuondoe tozo zote katika mafuta.” Kuhusu misamaha ya kodi mbunge huyo alisema kuwa inashangaza kuona kwamba wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CIG) alishauri misamaha ipinguzwe lakini Seikali inaongeza. “Katika misaha ya kodi hapa kuna vimemo vya wakubwa ni vingi, huyu mpe msamaha, Yule mpe msamaha,” alisema Zambi akiwatuhumu baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali kwa kuhusika na mashinikizo ya kusamehe kodi. Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba alisema kupandisha tozo katika ndege hakuendani na kasi ya sasa ya Serikali kujenga viwanja vya ndege maeneo mbalimbali nchini. “Hii itasababisha taifa kuwa na ndege mbovu jambo ambalo litasababisha ajali za ndege na kuwaumiza Watanzania.