Powered By Blogger

Translate

Friday, June 28, 2013

CAF YAHAIRISA MAANDAMANO


Dar es Salaaam. Chama cha Wananchi (CUF) kimeahirisha maandamano yaliyopangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu kwa sababu Rais Jakaya Kikwete, atakuwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Smart Partnership na kushughulikia ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani.
Maandamano hayo yalikuwa na lengo la kumfikishia Rais Kikwete ujumbe kuhusu vitendo vya ukatili, wizi, ubakaji na mauaji vinavyofanywa na polisi mkoani Mtwara na kutaka uchunguzi kuhusu matukio ya Arusha.
Hata hivyo kuahirishwa kwa maandamano hayo kunakuja baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote na kwamba polisi watapambana na yeyote atakayakaidi amri hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema: “Tumepokea barua kutoka Ikulu, kutuomba tusitishe maandamano hayo kwa sababu Rais ambaye ndiye mpokeaji wa maandamano hayo atapokea wageni mbalimbali watakaoingia nchini,” alidai.
Mtatiro alisema barua hiyo ilieleza kuwa haitawezekana Rais kupokea maandamano ya CUF kwa kuwa atakuwa akipokea wageni mbalimbali.
“Sisi tulimwandikia Rais barua kuwa Juni 29 mwaka huu tutakuwa na maandamano ya kuelekea Ikulu,hatukujua kama kutakuwa na ugeni wa marais siku hiyo...tumeahirisha,”alisema

CHADEMA YALIA NA HUJUMA


Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewatuhumu viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Jeshi la Polisi kwa kupanga njama ili kuwaunganisha viongozi wa juu wa Chadema kwenye kesi ya kumwagiwa tindikali, Mussa Tesha.
Viongozi waliotajwa hadharani kuwa wanapanga mbinu hizo ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba na Ofisa wa Jeshi la Polisi makao makuu, Advocate Nyombi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uenezi, John Mnyika alisema mikakati hiyo imesababisha kukamatwa kwa Katibu wa Chadema mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo wiki iliyopita na kupelekwa Igunga, mkoani Tabora  kuunganishwa kwenye kesi hiyo.
Kileo alikamatwa na kupelekwa makao makuu ya Jeshi la Polisi ambako alihojiwa na jopo la maofisa wa polisi. Kwa mujibu wa Mnyika baada kuhojiwa aliwekwa mahali pasipojulikana na kwamba alizuiwa kuwekewa dhamana.
Mnyika alisema siku iliyofuata, walielezwa kwamba Kileo alipelekwa Igunga kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka akituhumiwa kumwagia tindikali Tesha.
“Tumepata taarifa kwamba Kileo aliteswa vibaya na polisi ili awataje viongozi waliomtuma lakini alikuwa akibishana nao, lakini baadaye aliandikisha mambo waliyoyataka polisi,” alisema.
Akijibu tuhuma hizo, Nchemba alisema hakuna mikakati yoyote inayofanywa kati yake na Nyombi bali hiyo ni hofu yao viongozi wa Chadema kwa sababu wanafahamu kwamba walitenda kitendo hicho.
“Hatuhitaji kikao kudhihirisha hilo kwa sababu ni jambo lililo wazi kwamba Chadema walihusika katika kitendo hicho cha kumwagia tindikali mtu huyo,” alisema.
Kwa upande wake, Nyombi na Msemaji wa Polisi hawakupatikana kuzungumzia suala hilo, lakini Kamanda wa Mkoa wa Tabora, Peter Ouma alisema jeshi hilo litawasaka wahalifu popote walipo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria bila kujali kama ni wanachama wa vyama fulani au la.
“Mhalifu anaweza pia kuwa mwanachama wa chama fulani kwa hiyo tukimkamata tusihusishwe na mambo ya siasa bali ni kufuata sheria,” alisema kuongeza kuwa Kileo bado hajafikishwa mkoani humo.”
Chadema imeunda jopo la mawakili saba wakiongozwa na Profesa Abdallah Safari na wengine ni Peter Kibatara na Gasper Mwalyela wanaoondoka leo kwenda Igunga wakati Mabere Marando, Tundu Lissu, Nyaronyo Kicheere na Method Kimomogoro watawafuata baadae

NDEGE ZA OBAMA GUNZO


Dar es Salaam. Makachero wa Marekani wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama, ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na kazi ya kuunganisha helikopta za doria.
Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili.
Rais Obama tayari yuko katika ardhi ya Afrika, ambapo leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara yake ya kwanza Senegal na anatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa jana  unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili ya ulinzi wa Rais Obama, zikiwemo meli zilizobeba helikopta nyingine mbili na ndege.
Habari zilizopatikana kutoka kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,zinasema kuwa helikopta sita zinaunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpashaji mmoja  alisema kuwa helikopta hizo zililetwa kama vipande vipande vilivyosafirishwa kama mzigo kwenye meli za kivita zilizotia nanga jijini Dar es Salaam.
“Nilikaribia kwenye eneo la karakana na nikashangaa kuona jinsi jamaa walivyokuwa ‘bize’ wakiunganisha vyuma mbalimbali na kutengeneza helikopta hizo,” aliongeza mpashaji wetu, ambaye alibahatika kusogelea eneo hilo licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali.
Inaaminika kuwa helikopta hizo zitakuwa zinasaidia kusafirisha watu na mizigo kutoka kwenye meli za kivita ambazo zimeegeshwa kwenye Kikosi cha Maji cha JWTZ.
Pia helikopta mbili zinaaminika ziko katika meli ambazo zimeegeshwa huko Kigamboni.
Meli za kivita na ndege ya kijeshi
Katika hatua nyingine, meli mbili za kivita ambazo zimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu zimeegeshwa Kigamboni.
“Jamaa wana meli kali kwa kweli, mimi nimekuwa askari wa Kikosi cha Maji kwa muda mrefu na kufanya mazoezi na mataifa kadhaa, lakini sijaona meli kama zile

;OBAMA KUPATA PHD




Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.
“Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.
Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa.
Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka nchini Uingereza,David Mellor

MISRI APAFAI

Mahasimu wa kisiasa kuandamana Misri 28 Juni, 2013 Wapinzani wa Rais Morsi wanamtaka ajiuzulu wakati wafuasi wake wakimtetea Misri inajiandaa kwa maandamano ya mahasimu wa kisiasa kuhusu Rais Mohammed Morsi , huku maafisa wa usalama nao wakijikita mijini kudhibiti hali ya usalama. Taifa hilo linakumbwa na migawanyiko ya kisiasa na maandamano hayanishi huku pande pinzani zikitaka kuonyesha ubabe wao. Taarifa zinazohusiana Siasa Wafuasi wa Rais Mohammed Morsi wanajiandaa kufanya maandamano ya siku mbili kabla ya maandanao ya upinzani kumtaka rais Mosri kujiuzulu. Wakati huohuo, mtu mmoja aliuawa na wengine kujeruhiwa katika makabiliano Kaskazini Misri Alhamisi jioni. Bwana Morsi kwenye hotuba yake aliyoifanya mwaka mmoja tangu kuwa mamlakani, alisema kuwa maandamano yanatishia uthabiti na demokrasia ya Misri. Majeshi yameamrishwa kushika doria mjini Cairo na katika miji mingine. Bwana Morsi, ambaye ni mwanachama wa chama cha kiisilamu cha Muslim Brotherhood, ni rais wa kwanza wa chama cha kiisilamu kuwahi kuchaguliwa Misri. Mwaka wake wa kwanza mamlakani umekumbwa na ghasia na vurugu pamoja na maandamano ya kila mara huku uchumi nao ukiendelea kudorora. Baadaye leo maelfu ya wafuasi wa Morsi wanatarajiwa kufanya maandamano makubwa kumuunga mkono huku wakipinga matakwa ya upinzani kumtaka ajiuzulu. Baadhi ya makundi ya upinzani pia yanajiandaa kufanya maandamano baadaye mjini Cairo. Muungano rasmi wa upinzani, mnamo Alhamisi ulikataa wito wa rais kufanya mazungumzo nao. Kwenye taarifa yake chama cha National Salvation Front kilisema bado kinajiandaa kuitisha uchaguzi mkuu wa urais.

OBAMA ASIFU SENEGAL

Obama asifu Senegal kwa demokrasia 28 Juni, 2013 - Saa Obama anatarajiwa kwenda Afrika Kusini kisha Tanzania kwa ziara yake ya pili Afrika Rais wa Marekani Barack Obama ambaye yuko katika ziara yake ya Afrika, amesifu nchi ya Senegal kwa kuwa moja ya nchi zenye demokrasia thabiti barani Afrika. Akiwahutubia waandishi wa habari nchini Senegal kwa mkondo wake wa kwanza wa ziara yake Afrika,baada ya mazungumzo na rais Macky Sall, Bwana Obama alisema kuwa Senegal iliandaa uchaguzi huru na wa haki pamoja na kuwa na kipindi salama cha mpito. Taarifa zinazohusiana Siasa, Afrika Pia aliisifu kwa kuwa na mtindo wa kusuluhisha migogoro kwa mazungumzo na mashauriano, wala sio kwa njia ya ghasia. Alisema kuwa Afrika kama bara limepiga hatua kubwa upande wa demokrasia katika miaka ya hivi karibuni. Obama atazuru Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua sana na amelazwa hospitalini. Aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanamuombea Mandela pamoja na familia yake. Taarifa zinazohusia

MANDELA BABA WA AFRIKA

Dunia nzima inafuatilia afya ya raisi wa kwanya wa afrika kusini aliye lazwa hospitali kwa zaidi za wiki mbili sasa.Ni wazi kwamba hakuna matumaini ya ku Mandela bado anaugua sana hospitalini Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto. Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika. Taarifa zinazohusiana Afrika Kusini Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu. Awali mwanawe wa kike, Makaziwe amesema afya ya babaake inaendelea kuwa njema. Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake. Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi. "leo angalau yuko sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela. Bwana Zuma alifutilia mbali safari yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela hospitalini. Wakati huohuo mwanawe Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa. anae tena.Je nani atamrisi kwa ushujaa wake?