Askari Polisi na Mgambo wa Jiji wakiimarisha ulinzi katika eneo
lamanzese jijini Dar es salaam jana, baada ya kutokea vurugu kati ya
mgambo na Wamachinga zilizosababisha barabara ya Morogoro kufungwa kwa
muda kwa saa tatu.
Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni, Jordan Rugimbana amewataka wafanyabiashara ndogondogo
(wamachinga) kutodanganywa na wanasiasa kwa lolote kwani mpango wa
kuwaondoa maeneo wasiyotakiwa ni wa lazima. “Leo tunaendelea mitaa ya
Manzese, Ubungo na hata Mwenge kwani ni lazima waondoke ili kazi za umma
zifanyike’’ alisema.
Kauli ya Rugimbana imekuja ikiwa ni siku moja
baada ya kutokea vurugu za wafanyabiashara na polisi wa kutuliza ghasia
na mgambo wa jiji waliokuwa wakiwataka kuondoka katika eneo hilo ili
kutoa nafasi ya mradi wa ujenzi wa barabara wa mabasi yaendayo kasi
(BRT) eneo hilo.
Rugimbana alisema baadhi ya wanasiasa wanatumia
majukwaa yao vibaya kwa kuwadanganya wafanyabiashara hao hilo zoezi la
kuhamishwa eneo la Manzese ilikuwa ni la muda mfupi kwa ajili ya ujio wa
Rais Barack Obama. Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Rugimbana
alisema zoezi la kuwahamisha wamachinga hao ni la kisheria kwa sababu
lazima waondoke ili kumpisha mkandarasi aendelee na ujenzi wa barabara
hiyo.
“Tuna mgongano na baadhi ya wanasiasa ndio
wanaoturudisha nyuma wanawapotosha hawa wamachinga, sisi tunafuata
sheria sio siasa lazima waondoke ili mkandarasi aendelee kufanya kazi
eneo lile,” alisema Rugimbana.
Rugimbana alisema zoezi hilo ni endelevu hivyo
yeyote atakayeenda kinyume na agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria
hivyo wametakiwa kuondoka eneo hilo.
Alisema wafanyabiashara hao kama wana matatizo
wanatakiwa wamuone mkuu huyo, Meya wa manispaa hiyo ili waweze kukaa
pamoja na kutatua matatizo yao.
“Hili zoezi ni endelevu na leo hii oparesheni
itaendelea maeneo yote ambayo hayaruhusiwi kama Ubungo, Manzese na
Mwenge, kama eneo la Mwenge tumewaondoa wafanyabiashara na vibanda vyao
vimebomolewa ili kupisha upanuzi wa barabara,”

No comments:
Post a Comment