Wasomaji wangu ni matumaini yangu muu wazima wa afya na
mnaendelea vyema na majukumu mbalimbali ya
kujenga taifa na jamii zetu kiujumla.
Watanzania
tumeendelea kuishi kwa amani na furaha huku tukishuhudia ujio wa wakuu wa nchi
mbalimbali kuba hapa duniani.Tumeona raisi wa China akiwasili nchini na pia
raisi wa Marekani pia amefika nchini na msafara mkubwa. Wote wa hao wamepongeza
utawala uliopo tanzania na amani iliyopo.Watawala wa Tanzania wamebaki wakijisifu
kwamba wamedumisha utawala bora pengine kuliko nchi nyingine za Afrika.
Ni wakati
wetu watanzania kujiuliza je ni kweli kuna amani ya kudumu Tanzania? Na pia je
kuna utawala bora Tanzania?.Haya maswali magumu hayaweyi kujibiwa na viongoyi
walioko madarakani bali ni kwa sisi wananchi wa Tanzania kwa kutoa maoni na
fikra zetu.
Tukianza na
utawala bora,mtu akisema utawala bora ina maana ya utawala unaofuata sheria na
misingi uongozi na sheria na kanuni za nchi husika.Kwa ripoti mbalimbali na
matukio yanayoendelea Tanzania hatuwezi kusema kuna utawala bora nchini.Ufisadi
umekua kama hulka ya viongozi wetu kama
ule wa Richmond na dowans ,rada feki naule wa majengo pacha ya BOT.Pia kuna
ufisadi na ruswa iliyokisiri katika mahakama zetu,polisi na ngazi mbalimbali za
uongozi hapa Tanzania.
Licha ya ufisadi pia kuna suala la watu
kutungiwa kesi za uongo,watu kufungwa muda mrefu bila kufunguliwa mashitaka na
matendo mbalimbali ya kupeana ajira na huduma kwa kujuana na ucheleweshaji wa makusudi
wa huduma kwa wale raia wenye kipato cha chini.Ni waji bu wa wananchi kupigana
kupinga utawala mchafu usio jili matakwa ya wengi
Kikubwa
tulichonacho ni kuendelea kumshukuru mungu kwa kuendelea kutupa amani kwa zaidi
ya miaka hamsini sasa.Watanzania wamekuwa wavumilivu na kuendelea kuendelea
kutunza amani kwa nguvu zote.Swali linakuja na kuuliza amani hii itadumu mpaka
lini?.je watanzania wataendelea kuwa wavumilivu mpaka lini?.Mikono ya sheria
imewaona wanao jaribu kuvunja amani kwa nguvu zote?
Tumeona matukio mbalimbali kama kuuwawa kwa
padre kule Zanzibar,bomu kanisani Arusha,Mauaji yaliyo fanywa na polici Arusha,maandamano
kule Mtwara na harakati za shehe Ponda.Je haya yote yatanusuru amani iliyopo
nchini?.Je ni viashiria tosha vya kutokua na amani mwaka 2015.
Matatizo
yanayoendelea Brazil na Misri yamesababishwa na hali ngumu ya maisha na pia
utawala usiojali kama wetu hapa Tanzania.Hivi ni viashiria tosha kwamba kuna
kuanguka katika matatizo makubwa siku zijazo.
Ni rai yangu kwa viongozi wetu kutafuta
njia muafaka mapema kuondoa matatizo yaliyoko nchini mapema ili kuepusha taifa
kutumbukia mahala pabaya.Ni jukumu la wabunge bila kujali itikadi zao kupambana
kikamilifu kuishurutisha serikali iliyopo kulinda amani na kujali masilai ya
walio wengi.

No comments:
Post a Comment